Wahubiri marufuku kutafuta waumini kupitia TV na Redio

Add Comment

Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya imechapisha mwongozo mpya wa vipindi vya radio na televisheni.
Mwongozo huo unanuia kudhibiti nyakati za kupeperusha matangazo na vipindi vinavyolenga watu wazima na pia kuepusha matumizi ya lugha chafu na gumzo za ngono.
Mwongozo huo utakapotekelezwa pia utapiga marufuku kupeperushwa kwa vipindi vya kidini vyenye ujumbe wa kuomba pesa kwa waumini ili wapate baraka.
Mwaka uliopita, mhubiri mmoja aligonga vichwa vya habari baada ya makala ya ufichuzi kuonyesha akifanya miujiza bandia na kuwaomba watu wamtumie takriban $3 (£2) kupitia simu akisema ni baraka ndipo wapate baraka.
"Wahubiri hawafai kutumia dini kufaidi kutoka kwa watazamaji au wasikilizaji kwa kuwaomba wawasaidie kifedha au kushambulia imani ya mtu kwa kumshawishi mtu kubadili imani yake," mwongozo huo unasema.
Vipindi vya redio vinavyozungumzia ngono au masuala ya watu wazima, au kutumia lugha chafu pamoja na video zenye picha za uchi vyote havifai kupeperushwa kati ya saa kumi na moja asubuhi na saa nne usiku.
Hii ni mara ya kwanza hatua kama hiyo kuchukuliwa.
Kaimu mkurugenzi wa masuala ya wateja katika Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya Bw Christopher Wambua anasema mwongozo huo umeandaliwa baada ya majadiliano kati ya wadau mbalimbali mwaka jana.
"Mamlaka ilianza kutoa leseni za TV kwa mashirika mbalimbali baada ya kumalizika kwa kesi mahakamani ambayo ilikuwa imewasilishwa kupinga mamlaka ya mamlaka hiyo katika kudhibiti utangazaji. Mwongozo huu ni sehemu ya masharti ambayo watangazaji wanafaa kutii," Bw Wambua ameambia BBC.
"Mamlaka imewapa watangazaji miezi sita ya kutekeleza mwongozo huu. Muda huu utamalizika katikati mwa mwaka huu."
Orodha ya viongozi waliowahi tokwa machozi hadharani

Orodha ya viongozi waliowahi tokwa machozi hadharani

Add Comment

ObamaImage copyrightReuters
Image captionRais Obama ametokwa na machozi hadharani mara kadha
Rais wa Marekani aligonga vichwa vya habari alipotokwa na machozi alipokuwa akiwahimiza Wamarekani wakubali mabadiliko kwenye masharti ya uuzaji wa silaha Marekani Jumanne.
Alizidiwa na hisia alipokuwa akisimulia kuhusu shambulio la ufyatuaji risasi katika shule ya msingi ya Sandy Hook mwaka 2012 ambapo watoto 20 na watu wazima sita.
Hii haikuwa mara yake ya kwanza kutokwa na machozi akizungumzia kisa hicho.
Image copyright
Lakini kiongozi huyu hayuko peke katika kutokwa na machozi hadharani.
Wawafahamu hao wengine?
Machozi ya Olimpiki
Image copyrightty
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anajulikana pia kwa kutokwa na machozi hadharani.
Alibubujikwa na machozi mwaka 2009 baada ya mji wa Rio de Janeiro kutangazwa kwamba ungekuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016.
Machozi yake hayakuathiri umaarufu wake na ni mmoja wa marais waliopendwa sana katika historia ya aifa hilo.
Wasiwasi wa Karzai
Image copyright
Rais wa zamani wa Hamid Karzai aligonga vichwa vya habari duniani alipolia kuhusu hali ya Afghannistan wakati wa kutoa hotuba katika shule ya upili ya Kabul Septemba mwaka 2010.
Alitokwa na machozi alipokuwa akizungumzia mapigano nchini mwake, akisema alikuwa na wasiwasi kwamba hilo lingemfanya mwanawe kutorokea ng’ambo.
Kilio kikao cha wanahabari
Image copyrights
Video ya mwanasiasa wa Japan aliyelia baada ya kuulizwa maswali na wanahabari kuhusu matumizi yake ya pesa ilivuma sana mtandaoni Julai 2014.
Ryutaro Nonomura alitokwa na machozi alipotakiwa kujibu madai kwamba alikuwa ametumia pesa za umma kwa safari za kibinafsi.
Alisisitiza kwamba zilikuwa ziara za kikazi.
Baadaye alijiuzulu.
Machozi ya ushindi
Image copyright
Rais wa Urusi Vladimir Putin alionekana kutokwa na machozi alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake Manezhnaya Square, Moscow, baada ya kupata habari kwamba alikuwa ameshinda uchaguzi wa urais Machi 2012.
Machozi yake yalikuwa kinyume kabisa na sifa zake kama mtu mwenye roho ngumu na asiyetekwa na hisia. Baadaye, msemaji wa Putin alisema Putin alikuwa amezidiwa na upepo na baridi na wala si hisia zilizomteka.
Machozi ya kampeni
Image copyright
Wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais 2008 Hillary Clinton alitokwa na machozi akiwa New Hampshire, alipoulizwa na mwananchi, “Utafanyaje hayo?”
Suti yake ilibadilika na machozi kumtoka alipokuwa akimjibu.
Alifafanua baadaye: "Ningekuwa na wasiwasi sana kujihusu iwapo singekuwa na hisia kwamba hilo lilikuwa muhimu na la maana.”
Waziri huyo wa zaman wa mambo ya nje wa Marekani alitaka urais 2008 lakini akashindwa na Rais Barack Obama mbio za kumsaka mgombea wa chama cha Democratic.
Kuondoka madarakani
Image copyrights
Tarehe 28 Novemba 1990, Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo Margaret Thatcher alitokwa na machozi alipokuwa akitoa hotuba ya kuaga akiwa amesimama kwenye vidato vya jumba la Downing Street.
Kiongozi huyo wa kwanza mwanamke Uingereza, aliyejulikana kama Iron Lady, aling’atuka baada ya baraza lake la mawaziri kukataa kumuunga mkono uchaguzini.
Alionekana akitokwa na machozi, akipungia watu mikono kutoka kiti cha nyuma cha gari alipokuwa akiondoka afisini mara ya mwisho.

Magufuli, Lowassa wampongeza Samatta

Add Comment



Dar es Salaam. Si wanasiasa, si wanamichezo, wasanii na wengine wote walikuwa kitu kimoja wakati walipoungana kutoa salamu za pongezi kwa mshambuliaji nyota wa mpira wa miguu nchini, Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika.

Kundi hilo la wapeperusha salamu linaongozwa na Rais John Magufuli ambaye katika salamu zake za pongezi alizomtumia Waziri wa Michezo, Nape Nnauye, alisema; “tuzo hiyo imemjengea heshima Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medani ya soka la kimataifa”.

Pia, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikuwa miongoni mwa waliotuma salamu za pongeza akisema: “Ushindi wa Samatta ni changamoto kubwa kwa wanasoka wa Tanzania, lakini zaidi kwa Serikali kuwekeza kwenye eneo hilo.”

Samatta, ambaye anatarajiwa kuihama klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kujiunga na FC Genk ya Ubelgiji, alishinda tuzo hiyo ya Mwanasoka Bora wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa Wachezaji wa Barani Afrika juzi kwenye hafla iliyofanyika Lagos, Nigeria.

Mshambuliaji huyo, mwenye umri wa miaka 24, anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kutwaa tuzo hiyo baada ya kuiongoza TP Mazembe kutwaa ubingwa wa Afrika akiwa amefunga mabao sita.

Pia, ndiye mfungaji tegemeo wa Taifa Stars, akiwa amefunga mabao mawili kwenye raundi mbili za michuano ya awali ya Kombe la Dunia dhidi ya Malawi na Algeria, ingawa Stars ilitolewa kwa jumla ya mabao 7-2 na wababe hao wa Afrika Kaskazini.

Jana ilikuwa siku ya shangwe kwa Watanzania baada ya Samatta kutwaa tuzo hiyo usiku, baadhi wakituma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii na wengine taarifa kwenye vyombo vya habari kupongeza.

Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Dk Magufuli amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amfikishie salamu zake kwa nyota huyo.

Katika salamu hizo, Dk Magufuli amewasihi wanasoka wote na wadau kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.

Naye Lowassa, ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema, alisifu juhudi za Samatta.
“Huyu kijana kufikia hapo ni kujituma, lakini zaidi ni malezi aliyoyapata katika timu yake ya TP Mazembe... ni lazima tuwe na utaratibu wa kujenga shule za kukuza vipaji vya soka (academy), tutawapata akina Samatta wengi,” alisema Lowassa.

Alisema Serikali isione shida kuchukua ilani ya Chadema iliyoridhiwa na Ukawa ambayo inataka kufutwa kodi kwa vifaa vyote vya michezo.

“Wasione haya kuchukua ilani yetu. Sisi tulitangaza kuwa tutafuta ushuru kwa vifaa vyote vya michezo pamoja na kuanzisha academy ili kuinua vipaji. Tunaamini kwa kufanya hivyo watapatikana akina Samatta wengi tu na si katika soka, bali hata michezo mingine kama riadha na ngumi.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, ambaye ni shabiki maarufu wa klabu ya Yanga, aliandika kwenye ukurasa wake wa Tweeter kumpongeza Samatta akisema ushindi wake umeipa heshima nchi.

“Hongera sana, ufanikiwe zaidi ya hapa,” alisema Nchemba katika ujumbe wake.
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika naye hakuwa nyuma kumwagia sifa Samatta, akisema mafanikio yake yanadhihirisha pasi na shaka uwepo wa vipaji lukuki hapa nchini ambavyo hupotea bila kufikia ukomo wa juu wa ndoto na uwezo wao.

“Tunahitaji mikakati sahihi, utekelezaji na uwekezaji wa kutosha katika soka. Inawezekana! Tuiangalie hii kama fursa ya kuwakwamua vijana wetu kuzalisha ajira na wao kutimiza ndoto na matamanio yao,” alisema Mnyika katika salamu zake.

‘Kufeli mtihani si kufeli maisha’
Nyumbani kwa wazazi wa Samatta na shuleni kwake ilikuwa ni kutafakari safari ya mshambuliaji huyo tangu utotoni.

“Haya ni mafanikio makubwa,” alisema mwalimu wa michezo wa Shule ya Sekondari ya Thaglan ya Mbagala, Mapesi Jamal ambaye hivi sasa amehamishiwa Kisiju wilayani Mkuranga.
“Niligombana naye sana nikitaka apende vitu vyote viwili (shule na mpira) kutokana na kutokuwa vizuri darasani, ndiyo maana matokeo yake ya mwisho hayakuwa ya kuridhisha.
“Nakumbuka (baadaye) niliwahi kumwambia ajitahidi sana kupenda mpira na uwe ndiyo chaguo lake la kwanza baada ya kugundua kuwa darasani ameshindwa.

“Tangu ajiunge kidato cha kwanza alikuwa tayari ameanza kujifunza soka kwenye kituo cha Jamal Kisongo alikokuwa akichezea timu ya vijana ya klabu ya Mbagala Market.”
Mwalimu Mkuu wa Thlagan, Juma Nyenga ambaye kwa sasa ni mlezi na mshauri wa shule hiyo, alimwelezea Samatta kuwa ni kijana mpole ambaye hakukatishwa tamaa na matokeo mabaya ya kidato cha nne.

“Alionyesha njia nyingine ya kupata mafanikio ambayo ni soka,” alisema Nyenga.
Nyange aliiambia Mwananchi kuwa wamefurahishwa na mafanikio ya Samatta kwa kuwa yanamtangaza yeye, shule na nchi yake.
Alisema kuna kipindi aliingia kwenye matatizo ya kitaaluma na walilazimika kumuita baba yake shuleni.

“Mzee Samatta ni muelewa pia, alituambia mfumo wa mwanaye na kutuomba tumsaidie jinsi ya kuendesha maisha yake kwa kuwa tayari ameonyesha kuwa alikuwa anapenda soka kuliko shule. Ingawa hata sisi tulitaka apende vitu vyote kwa pamoja, nililazimika kumpa adhabu ya kumchapa viboko vinne mbele ya mzazi wake,” alisema.

Nyenga anasema tangu siku hiyo alirudisha mapenzi ya kuhudhuria vipindi.
Walimu hao wanaona Samatta bado hajachelewa kujiendeleza kielimu.
“Tunaposema arudi darasani si kwenda kusoma masomo yote upya, kwa vile amekuwa ni wa kimataifa na matokeo yake hayakuwa ya kuridhisha, anatakiwa kujiendeleza kwa kusoma lugha ya Kiingereza,” alisema

“Pia kama ameweza kufuata miiko ya soka, basi anatakiwa aendelee hivyohivyo maana hiyo pekee ndiyo itampa mafanikio zaidi huko mbele. Awe na nidhamu si uwanjani pekee, hata nje ya uwanja kama alivyo sasa, awekeze kwani mpira una muda wake,” alisema Mapesi.


Baba amwaga machozi
Baba yake mzazi, Ally Samatta alisema aliangua kilio mara baada ya mwanaye kutangazwa mshindi.
“Nilifuatilia kuanzia mwanzo hadi mwisho. Walipotangaza sikuamini, nilijikuta naangua kilio mpaka majirani walishtuka,” alisema mzazi huyo.
“Nimefurahi na ninampongeza sana kwa hilo, pia nawashukuru Watanzania wote waliowezesha hili kwa njia moja au nyingine.

“Nilimpa maneno ya siri alipokuwa anakwenda huko na hata atakaporudi nitamwambia. Nashukuru huwa anazingatia. Samatta amekuwa mchezaji bora kama nilivyokuwa mimi mwaka 1964 nilipotwaa tuzo hiyo kwa Tanganyika ila yeye kanifunika kabisa.”

Mama mlezi wa Samatta, Khadija Abdallah naye alikuwa na furaha.
“Mimi nilijikuta presha inapanda huku kichwa kikiniuma sana, hatujalala kabisa kwani bado hatuamini kwa kweli. Tumelala saa 11 alfajiri na tumeamka saa moja asubuhi,” alisema.
Mzee Samatta alitoa ahadi kwa mwanaye kuwa akitwaa tuzo hiyo basi watamfanyia sherehe kubwa.
Wazazi hao wameeleza kuwa mtoto wao anapokuwa likizo huwa anapendelea kufanya mambo kadhaa, hasa usafi wa nyumba, kuangalia televisheni, kucheza game, kusikiliza redio pamoja na kuchati.

Wazazi wake walisema Samatta alikuwa anamiliki nyumba saba, lakini moja ambayo ipo Saku, Maji Matitu ameibomoa na ana mpango wa kujenga msikiti, nyingine iliyokuwa Mbande aliiuza kwa sababu ilijengwa chini ya kiwango hivyo amebaki na nyumba tano.
Mbali na nyumba hizo anamiliki viwanja zaidi ya 10 pamoja na mashamba zaidi ya matatu na magari ya kifahari.

Imeandikwa na Boniface Meena, Mwanahiba Richard na Olipa Assa (Mwananchi Communications)

Mfumuko wa bei wazidi kutishia

Add Comment


Dar es salaam. Mfumuko wa bei za bidhaa umeongezeka kutoka asilimia 6.6 hadi kufikia asilimia 6.8 Desemba mwaka jana sababu kubwa ikiwa ni ongezeko la bei kwa bidhaa za vyakula.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo alisema mfumuko wa bei za bidhaa kwa Desemba, mwaka jana umechangiwa na mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonyesha kuongezeka ikilinganishwa na bei za Desemba 2014.

Alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8 kwa Desemba ikilinganishwa na 0.5 kwa Novemba.
“Bidhaa zilionyesha kuongezeka bei katika kipindi cha Desemba ni pamoja na bei za mchele kupanda hadi kufikia asilimia 28.2, mahindi kwa asilimia 16.4, unga wa mahindi asilimia 11.1 nyama asilimia 11.3, samaki asilimia 8.9, maharagwe asilimia 9.7 na viazi kwa asilimia 20.2.”

Vilevile, alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonekana kuongezeka ikilinganishwa na bei za Desemba 2014 ni pamoja na bei za mavazi kwa asilimia 4.9, huduma za afya asilimia 11.1 vyakula kwenye mighahawa asilimia 8.3 na gharama za malazi kwa asilimia 6.8.

Hata hivyo, alisema uwezo wa Sh100 ya Tanzania kununua bidhaa na huduma umefikia Sh62.02 kwa Desemba mwaka jana ikilinganishwa na Sh62.31 ilivyokuwa Novemba mwaka jana.

Alisema mfumuko wa bei za bidhaa nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya bidhaa za nchi nyingine Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na ongezeko la asilimia 8.01 Kenya kutoka asilimia 7.32 kwa Novemba na Uganda ongezeko la asilimia 9.30 kutoka 9.18 Novemba mwaka jana.

Makampuni 980 kuilipa Serikali Sh16 bilioni

Add Comment
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk Servaciaus Likwelile



Dar es Salaam. Serikali inatarajia kukusanya Sh16 bilioni kupitia kampuni zaidi ya 980 zilizokopeshwa fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na malighafi kutoka nje ya nchi katika kipindi cha mwaka 1980 hadi 2004.

Kiasi hicho cha fedha kitakusanywa na Kampuni ya M/S Msolopa Investment Ltd iliyoingia mkataba wa miaka miwili na Wizara ya Fedha na Mipango.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana na Wizara hiyo, fedha hizo zilitolewa kupitia wahisani mbalimbali kwa ajili ya mpango maalumu uliofahamika kama ‘Commodity Import Support’ (CIS) uliolenga kuipatia Serikali uwezo wa kuimarisha uchumi wake kupitia taasisi, kampuni, viwanda na biashara mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msolopa Investment Co Ltd, Ibrahim Msolopa alisema ni mara ya pili kwa kampuni yake kuingia mkataba na wizara hiyo, wa kwanza ulikuwa mwaka 2008 hadi 2011.

“Mkataba wa kwanza tulikusanya Sh4 bilioni kutoka kampuni 70, lakini baadaye tulisitisha mkataba kutokana na wizara kurekebisha sheria ambayo hapo awali ilikuwa hairuhusu sisi kumkamata mtu ambaye amekaidi kulipa, lakini baada ya sheria hiyo kuboreshwa sasa tuna uwezo wa kumkamata,” alisema Msolopa.

Hata hivyo, katika tangazo hilo lililosainiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Servacius Likwelile, linaeleza kuwa hata kama mkopaji alichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18, mkopo huo unakuwa na kufikia asilimia 17.

CIS ni Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi, ambao ulikopesha fedha za kigeni kwa baadhi ya wafanyabiashara wazalendo.

Mpango huo ulianzishwa na Serikali katika miaka ya 1980 na kudumu hadi mwaka 2000.
Fedha zake zilitoka nchi wahisani ikiwamo Japan, Uingereza, Uholanzi, Saudi Arabia, Uswis, Norway, Denmark na Ubeligiji.
Lengo la fedha hizo za kigeni ilikuwa ni kuimarisha sekta ya biashara.

Askofu Pengo kuruhusiwa leo

Add Comment


Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo imeimarika na leo ataruhusiwa.

Kardinali Pengo alifikishwa katika hospitali hiyo Desemba 31, mwaka jana kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Profesa Janabi alisema Pengo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo. Hata hivyo, hakueleza kwa undani.

Jana, kwa mara ya kwanza tangu afikishwe katika hospitali hiyo, Pengo alijitokeza hadharani na kuzungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo na waandishi wa habari, huku akishukuru kwa huduma alizopata.

Alisema amepatiwa huduma nzuri na kumfanya afute kichwani mwake habari za watu mbalimbali wanaodai kuwa MNH haiwahudumii vizuri wagonjwa.

“Nataka niwashukuru wahudumu wote walionifikisha katika hali hii, hasa Profesa Janabi na Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga,” alisema.

Akiwa hospitalini hapo jana, Kardinali Pengo alitembelewa na maaskofu wasaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe na Eusebius Nzigilwa pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Damian Dallu.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali imejipanga kuhakikisha wagonjwa wa moyo hawapelekwi nje ya nchi kutibiwa.
Alisema tangu kuanza kwa mpango wa kuwatibu wagonjwa hao nchini Taifa limeokoa takribani Sh5 bilioni.

“Tutatoa vibali kwa wagonjwa kutibiwa nje ya nchi ikiwa itathibitishwa na madaktari kuwa huduma husika haiwezi kutolewa nchini,” alisema. Jana, Profesa Janabi alisema waliwahudumia wagonjwa 500 na mwaka huu wanatarajia kupokea kundi la madaktari bingwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutoa mafunzo.

Waamuzi Bongo watupwa nje CHAN

Add Comment


MWAKA 2009, Tanzania iliweka rekodi ya kuvutia baada ya kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).


Michuano hiyo mipya iliyofanyika wakati huo mara ya kwanza nchini Ivory Coast, lengo lake ni kuwapa nafasi wachezaji wa Afrika wanaocheza ligi za ndani kuwa na mashindano yao makubwa yenye hadhi.


Pengine kwa kutambua kwamba mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) hutawaliwa na mastaa wengi wanaocheza nje ya Afrika hasa Ulaya, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likaja na wazo la kuanzisha CHAN.


Hata hivyo tangu wakati huo, Tanzania haijapata tena nafasi ya kushiriki mashindano hayo licha ya kushiriki mara zote katika hatua za awali za kuwania kufuzu hali ambayo kimsingi haipendezi kwa taifa kubwa kama Tanzania.


Mashindano ya CHAN, bado machanga hasa kwa kuwa hayajafikisha hata miaka 10 hadi sasa na ni wazi kwamba kadri siku zinavyokwenda ndivyo yatakavyozidi kuwa makubwa

Mwaka huu, mashindano hayo yanafanyika nchini Rwanda na mbali na Tanzania kushindwa kufuzu, bado kuna eneo lingine ambalo Tanzania imetupwa katika mashindano hayo.


Pamoja na uchanga wa CHAN lakini Tanzania pia imetupwa kwenye waamuzi, katika orodha ya waamuzi iliyopatikana hivi karibuni wametajwa waamuzi zaidi ya 20 huku jina la mwamuzi wa Tanzania likikosekana.


Hili ni jambo ambalo limetugusa na ingawa hatutaki kuingia kwa undani kuhusu vigezo lakini jambo moja linalokuja katika fikra ya kila mdau wa soka ni swali la kwanini waamuzi wa Tanzania hawamo.


Akikosekana mwamuzi kwenye Kombe la Dunia au Afcon kidogo jambo hilo linaweza kuonekana la kawaida lakini katika CHAN, mashindano ambayo ni machanga wadau wa soka wana haki ya kujiuliza.


Ni kwa mtazamo huo huo tunapenda kuwakumbusha waamuzi nchini wajiulize nini hasa tatizo, ni kwanini waamuzi wa Tanzania hawamo kwenye CHAN.

Waamuzi watafakari jambo hili kwa mapana ili wajue nini hasa kilichowakwaza kiasi cha kukosa nafasi ya kuwamo kwenye CHAN hasa baada ya timu ya Tanzania kushindwa.


Mbali na maslahi ambayo mwamuzi anaweza kuyapata kwa kuwa katika mashindano haya lakini kama nchi ni heshima ya kipekee, kila Mtanzania bila kujali ni shabiki au si shabiki wa soka anafarijika kuona mwamuzi wa Tanzania akipeperusha bendera nje ya nchi.

Teknolojia: Choo kinachojifungua na kujiosha

Add Comment

Choo cha kisasa ambacho kina uwezo wa kujifungua unapokaribia na pia kujiosha, ni moja ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya teknolojia mpya za bidhaa za elektroniki Las Vegas.
Choo hicho, kilichopewa jina Neorest, pia humsafisha anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa mtu akiwa ameketi.
Kina pia teknolojia inayokiwezesha kuua bakteria na virusi.
Licha ya choo hicho kuuzwa $9,800 (£6,704), waliotengeneza choo hicho vyoo zaidi ya 40 milioni vya miundo ya awali vimeuzwa.
Kampuni ya Toto, iliyotengeneza choo hicho, imesema muundo huo wa sasa bado unaendelea kuboreshwa.
"Huhitaji kuosha bakuli la choo kwa kipindi cha mwaka mmoja,” anasema msemaji wa Toto, Bi Lenora Campos.


Image copyrightr

Choo hicho hata hivyo si kwamba kitakuondolea kabisa majukumu yote ya usafi chooni, kwani hakiwezi kujiosha upande wa nje iwapo kutakuwa na uchafu.
Maonyesho hayo ambayo kwa Kiingereza yanajulikana kama Consumer Electronics Show hufanyika kila mwaka ambapo kampuni mbalimbali na wavumbuzi huonyesha teknolojia za karibuni zaidi.

BALE Kutua Trafford?

Add Comment



MANCHESTER, ENGLAND

RYAN Giggs ametumwa kazi ya kumshawishi Gareth Bale ajiunge na Manchester United katika dirisha la usajili wa Januari hii.


Bale yupo tayari kung’oka Real Madrid baada ya kocha aliyekuwa akimkubali sana na kumwacha huru ndani ya uwanja, Rafael Benitez, kutimuliwa kazi Jumatatu iliyopita, hivyo maisha yake yatakuwa kama ilivyokuwa chini ya Carlo Ancelotti.


Kocha mpya, Zinedine Zidane amemtuliza Bale akimweleza kwamba bado atapata nafasi kwenye kikosi chake baada ya kupewa mikoba wiki hii, lakini hilo haliwezi kumzuia staa huyo wa Wales kuachana na maisha ya Bernabeu.


Bale amefichua kwamba yupo tayari kurudi kwenye Ligi Kuu England huku Man United ikidaiwa kuwa na mipango thabiti na winga huyo.


Hata hivyo, Man United italazimika kulipa kiasi cha Pauni 150 milioni kuinasa sahihi ya winga huyo ambaye alisajiliwa Real Madrid kwa Pauni 85 milioni kutoka Tottenham Hotspur miaka mitatu iliyopita.


Bale amemwambia Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, kwamba alikuwa na uhusiano mzuri na Benitez, hivyo kuondolewa kwake kutakuwa na athari kubwa kwenye maisha yake ya soka.

Man United ilitumia wiki kadhaa kwenye dirisha lililopita la usajili kumtaka mchezaji huyo, lakini Perez hakuwa tayari kumuuza staa huyo na alisema labda kwa ada ya Pauni 150 milioni, huku mshahara wa mchezaji huyo akitaka uanzie Pauni 300,000 kwa wiki.


Bale anataka kuondoka, lakini Perez anagoma kumuuza, huku miamba hiyo ya La Liga ikipiga hesabu za kumsajili winga, Eden Hazard.


Zidane alisema: “Naelewa, Bale atakuwa ameumizwa sana kwa kuondoka Benitez kwa sababu alikuwa kocha muhimu kwake. Lakini, chini yangu bado atakuwa muhimu kama alivyokuwa kwa Rafa.


“Ni mchezaji muhimu kwenye kikosi, muhimu kwa timu. Ni wa aina yake na amekuwa matata sana katika siku za karibuni. Nitampa sapoti, hivyo ataendelea kucheza vizuri tu.”

Bale amefunga mabao saba katika mechi saba zilizopita na anataka kuendelea kupewa nafasi muhimu kwenye kikosi kwa sababu inamfanya kuwa bora zaidi uwanjani.

Waliokuwa wakila nyasi na udongo Syria wapata msaada

Add Comment

Umoja wa Mataifa umesema serikali ya Syria imekubali kuruhusu misaada ya kibinadamu kwenda katika mji ulizingirwa wa Madaya ambayo kuna taarifa watu wamekuwa wakifa kwa njaa.
Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limeiambia BBC kuwa msafara wa umeingia katika mji ulikuwa ukikaliwa na waasi katibu na mpaka na Lebanon.
Madaya ulilkuwa umezingirwa na majeshi ya serikali na wafuasi wao wa Hezbollah kwa miezi kadhaa picha za video katika eneo hilo zinaonyesha watu wakiwa katika hali mbaya. Inaelezwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakilazimika kula majani na udogo badaa ya chakula kumalizika.
Mkuu wa shirika la chakala duniani katika ofisi za London Grey Barrow amesema maandalizi yanafanyika kuhakikisha misaada inawafikia wanaohitaji.
"Kumekuwa na mipango inayofanyika kabla ya magari kuingia eneo hilo labda inaweza kuwa ndani ya saa sabini na mbili labda hilo ndilo linaweza kuwezekana. Ninaamami hadi jumatatu tutapeleka magarai eneo hilo magari ambayo yapo tayari lakini yanahitaji mipango."
Hata hivyo Grey ametahadharisha eneo wanalopeleka misaada ni eneo la hatari.
"Nadhani ni lazima tukubali tunakoenda hali ni mbaya. Tunakwenda eneo la mstari wa mbele tunapaswa kujua tunapoingia pale hakuna hatari ya kudhurika, kwamba tutapeleka chakula huko na mahitaji mengine tutakayobeba kwa niaba ya mashirika mengine ya kibinadamu na tunadhani tutawafikia wale wenye mahitaji makubwa."

Wapalestina wanne wauawa Israel

Add Comment

Wapalestina wanne wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kujaribu kuwadunga visu wanajeshi wa Israel katika visa viwili tofauti, jeshi la Israel limesema.
Visa hivyo vilitokea eneo la Ukingo wa Magharibi.
Watatu waliuawa katika makutano ya barabara ya Gush Etzion, ambako visa kama hivyo vimewahi kutokea awali. Wa nne aliuawa karibu na Hebron, jeshi limesema.
Hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa.
Maafisa wa afya wa Palestina wamethibitisha vifo hivyo.
Vyombo vya habari Palestina vimetaja watatu hao kuwa Muhanad Kawazbeh, 20, Ahmed Kawazbeh, 21, na Alaa Kawazbeh, 20, wote kutoka kiji cha Sair, kaskazini mashariki mwa Hebron.
Wa nne ni Khalil Shalalda, 16, pia kutoka Sair.
Kumekuwa na ongezeko la visa vya mashambulio kati ya Waisraeli na Wapalestina miezi ya hivi karibuni.
Waisraeli 22 na Wapalestina zaidi ya 140 wameuawa tangu 1 Oktoba.
Waisraeli hao wameuawa kwa kudungwa visu, kupigwa risasi na kugongewa magari.
Nusu ya Wapalestina waliouawa wamedaiwa na Israel kuwa washambuliaji. Wengine wameuawa kwenye makabiliano na maafisa wa usalama.

Amani Karume, Lipumba wahudhuria Maulid kwa Maalim Seif

Add Comment


Zanzibar. Rais wa awamu iliyopita wa Zanzibar, Dk Amani Abeid Karume amehudhuria hafla ya Maulid iliyoandaliwa na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad katika kipindi ambacho Zanzibar inahaha kutatua mgogoro wa kisiasa uliotokana na Uchaguzi Mkuu.

Hafla hiyo, ambayo pia ilihudhuriwa na Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omary Kabi, iliandaliwa na mgombea huyo wa urais wa Zanzibar na kufanyika kwenye Hoteli ya Bwawani mjini hapa.
Zanzibar iliingia kwenye mgogoro wa kisiasa baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani, kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi.

Alitangaza kuwa uchaguzi huo utarudiwa ndani ya siku 90 na tangu wakati huo kumekuwa na mazungumzo ya kutafuta suluhisho la mgogoro huo yanayomuhusisha Maalim Seif, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na makada wengine watano, akiwamo Dk Karume.
Pamoja na Maalim Seif na Dk Shein kuwa kwenye mazungumzo hayo ya kutafuta suluhisho, kumekuwapo na kurushiana maneno baina ya CCM na CUF kuhusu uamuzi wa mazungumzo hayo, na juzi yalichukua sura mpya baada ya rais huyo wa Zanzibar kujitangaza kuwa ndiye kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, akiwataka wasioamini kwenda mahakamani.

Jana kwenye hafla hiyo, Maalim Seif alipata nafasi ya kumjibu Dk Shein ingawa hakueleza moja moja kauli yake kwa rais huyo wa Zanzibar.

“Nawasihi muendelee kuwa watulivu wakati huu ambao nchi yetu imekabiliwa na mkwamo wa kisiasa. Naamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutaweza kukwamuka, Inshaallah,” alisema Maalim.

Kwenye hafla hiyo, Maalim Seif, ambaye amekuwa akieleza kuwa ndiye aliyeshinda kwenye uchaguzi huo, aliwataka Wazanzibari kutobabaishwa na maneno ya baadhi ya watu wanaotaka kuwavunja moyo na kuwataka wawe watulivu. Imekuwa nadra sana kwa viongozi wa CCM, hasa aliyewahi kushika nafasi ya juu kama Dk Karume kuhudhuria hafla za wapinzani visiwani Zanzibar ambako upinzani wa kisiasa ni mkubwa, ingawa shughuli ya jana iliandaliwa na familia ya Maalim Seif.

Mwaka jana, mmoja wa waasisi wa Muungano, Nassor Moyo alitimuliwa uanachama wa CCM kwa madai kuwa amekuwa akihudhuria mikutano ya CUF na kuhutubia.

CUF inadai kuwa Dk Shein si rais tena wa Zanzibar kwa kuwa muda wake uliisha tangu nchi ilipopiga kura kumchagua, lakini CCM inamtetea kuwa ndiye mwenye haki ya kuendelea kuongoza hadi Rais mpya atakapochaguliwa.

Wakati CCM inawataka wafuasi wake kuanza kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi, CUF imekuwa ikieleza kuwa ZEC inatakiwa imtangaze mshindi wa uchaguzi na haitakuwa tayari kurudia kupiga kura.

Chadema kujitathimini upya

Add Comment


Dar es Salaam. Siku 74 baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kimefanya kikao cha kujitathmini na kuweka mpango kazi kwa miaka mitano ijayo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana, mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa alishindwa na Rais John Magufuli wa CCM aliyepata kura Milioni 8.8 sawa na asilimia 58.5.

Lowassa alipata kura Milioni 6 sawa na asilimia 39.97 ya kura zote.
Chadema pia ilipata wabunge 70, wakiwamo 36 wa viti maalumu huku CCM ikipata wabunge 188. Katika chaguzi ndogo saba zilizofanyika baada ya uchaguzi huo mkuu, CCM iliongeza wabunge takribani tisa, wakiwamo wa viti maalumu watatu na Chadema mbunge mmoja wa kuchaguliwa.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho jana, ilieleza kuwa itajadili vipaumbele vyake vya mwaka 2016-2020 na kuwasilisha katika kikao cha kikatiba na uamuzi kwa ajili ya utekelezaji.

“Lengo ni kukiimarisha chama na kuiondoa CCM madarakani ili kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli kuliko haya yanayofanyika sasa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa moja ya ajenda ilikuwa ni kubadilishwa kwa idara za chama hicho kwa ajili ya kujipanga kwa ajili ya mkutano ujao wa Bunge.

“Pia, watajadili tamko la Waziri Mkuu, Kassim (Majaliwa) la kuzuia mikutano ya vyama vya siasa,” ilieleza taarifa hiyo.

MAKALA: Jinsi ya kujipanga 2016 kwa mafanikio endelevu

Add Comment

Bila shaka wasomaji wangu bado mnaendelea kusherekea Mwaka Mpya wa 2016 baada ya kuvuka 2015. Ni vizuri kujipongeza na kutafakari ulifanya nini mwaka jana.

Ni vyema ukafahamu kuwa ulikuwa wa mafanikio au wa hasara? Je, mipango yako uliyojiwekea umefanikiwa ?, bila shaka majibu ya maswali hayo ndiyo yatakayotoa dira yako ya mwaka huu wa 2016.

Kama ulifanikiwa una kila sababu ya kujiimarisha ili mambo yaendelea kuwa hivyo 2016. Kama hukufanikiwa ni wakati wa kuweka mikakati ya mafanikio. Lazima kila mtu kuhakikisha unapiga hatua mbele ya maendeleo.

Kuwa na mpangilio wa utekelezaji. Jambo lisilokuwa na mpangilio unaoeleweka, mtiririko mzima husababisha jambo kuchukua muda mwingi kufanikishwa. Hivyo kuchelewa kimaendeleo.
Maendeleo ninayozungumzia hapa ni yale ya kiuchumi kwa ajili ya wakati huu na ya muda mrefu ujao. Ni wazi tunakabiliwa na majukumu mengi kuanzia ya binafsi, familia na jamii inayotuzunguka. Yote hayo ni mambo ambayo mtu anapaswa kuyatatua kwa hali na mali. Niliwahi kuandika makala juu ya hali halisi kwamba kutofikiri leo umempa mtu nafasi akufikirie na kisha kukutawala pasipo wewe kufahamu. Ndugu yangu, binadamu wote ni sawa, ila tunafanyaje ili kuutimiza huu usawa?
Wachunguzi wa mambo wanasema asilimia tatu ya watu duniani wana malengo. Wameweka mikakati ya namna ya kuwa na mafanikio tena kwa kuyaandika ama kuyaorodhesha na kupanga nini kianze na kipi kimalizikie.

Asilimia 97 ya watu duniani hawana malengo maishani mwao. Kwa lolote tu lile likitokea basi, na wao humohumo. Kwa kifupi ni kusema mafanikio kwao yanapatikana kwa kubahatisha tu.
Hii inatokana na kukosa muda wa kufikri ili wajikomboe. Kuna mambo niliwahi kujifunza kwa wanazuoni mbalimbali, mmojawapo ni Dk John Maxwell katika kitabu chake cha “Thinking for Change”. Kuna jinsi mbalimbali za kufikiri ambazo zina tija kama ukiwa makini.

Moja ni kufikiri kwa zingatio jambo moja. Ina maana ondoa mambo mengine yote, fikiria ama tafakari jambo moja. Uwezo wa kufikiri kwa kuondoa mambo yanayochanganya kwenye akili yako, kutakusaidia kulinyambua jambo husika kwa kina.

Hatua ya pili ni kufikiri kwa ubunifu. Jambo la tatu ni kufikiri kimkakati. Panga ratiba au mkakati wa utekelezaji wa mipango yako. Jambo unalopaswa kuzingatia pia ni kuzingatia suala la muda. Tumia muda vizuri. Muda ni hazina ambayo ikipotea hairudi tena na pia lazima mtu anayepoteza muda siku atakuja kuulipia kwa namna yeyote ile.

Wanadamu wote tuna saa 24, je, umeshawahi kujiuliza katika muda huo umeutumia vipi kutengeneza vitu vipya au kuongeza thamani katika maisha yako?
Ukiona una majukumu mengi kiasi kwamba huwezi kutekeleza yote katika saa 24 ili kuharakisha maendeleo jipange kuajiri watu wa kukusaidia kufanikisha hayo. Mtu aliyewekeza huajiri watu ili wafanikishe lengo la faida aliyokusudia.

Je, wewe muda wako wa saa 24 una kutosha? Kama siyo je huo muda ambao haukutoshi unautumia kwa ajili yako zaidi au unautoa bure kuangalia runinga, tamthilia, kupiga simu zisizo na masilahi, kuingia na kukaa mitandao ya kijamii siku nzima?

Kama haupo makini katika kutumia muda wako jua una deni kwa sababu ya kuja na kuishi hapa duniani. Kuna sababu ambazo husababisha watu wengi kushindwa kuutawala muda vyema.
Kutokuwa na malengo. Ni ngumu kufanikisha jambo kama hujaweka malengo ambayo yanaeleweka mfano nini unataka, lini, wapi, kiasi gani na kadhalika.

Jifunze pia namna ya kupata mafanikio. Hapa unapaswa kujifunza kuwa bingwa wa kutumia muda na siyo kusema; ‘muda si rafiki.’ Weka kumbukumbu ya mambo yako na uwe na muda wa kutathmini juu ya yale uliyoyafanya. Tafuta muda wa utulivu ili utafakari juu ya mipango yako.

Mtu anayetafakari mambo ana faida kubwa nyingi. Mojawapo ni kuepuka kutumia muda mwingi wa ufanyaji jambo fulani kwa kuwa hutumia kanuni. Katika hali hiyo huwa na uwezo wa kujiamini vya kutosha kwa sababu ni jambo la msingi ambalo limejengwa kwa kutokurupuka.
Wiki ijayo nitaelezea maeneo ambayo mtu akiwekeza mwaka huu ana nafasi kubwa ya kupata mafanikio.

Na; Deogratius Kilawe,Mkurugenzi wa Excel.

Meneja apinga bomoabomoa

Add Comment

Dar es Salaam. Wakati Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) likiendesha bomoabomoa katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam, Abdallah Bulembo, aliyekuwa meneja kampeni wa Rais John Magufuli amepinga operesheni itakayofanyika nje ya maeneo ya Bonde la Msimbazi na amemshauri Rais aingilie kati ili isitishwe.

Bomoabomoa hiyo, inayolenga nyumba zilizojengwa mabondeni, kwenye fukwe za bahari, kingo za mito na maeneo ya wazi, imekuwa ikipingwa vikali na wamiliki na wakazi wa nyumba hizo kwa maelezo kuwa hawakupewa taarifa na hawajaandaliwa sehemu mbadala ya kwenda.

Wakazi hao wamefikia hatua ya kumlaumu Rais Magufuli kwa kutojitokeza na kukemea ubomoaji huo, ambao katika baadhi ya maeneo umesimamishwa na Mahakama Kuu kwa muda.
Jana, Bulembo, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, aliiambia Mwananchi katika mahojiano maalumu kuwa anakubaliana na bomoabomoa inayofanyika Jangwani na maeneo hatarishi ya Bonde la Msimbazi, lakini akaitaka NEMC kuacha kubomoa nyumba ambazo haziko kwenye bonde hilo.

Bulembo, ambaye aliambatana na Rais Magufuli kwa siku 52 katika kampeni za urais alisema kuwa operesheni hiyo inamjengea chuki Rais Magufuli kwa wananchi.
Bulembo, ambaye alikuwa na mazungumzo na Rais Jumatatu wiki hii, alisema kuendelea kuwabomolea wananchi nyumba walizokuwa wakiishi miaka mingi, ni kuvuruga imani waliyonayo kwa kiongozi huyo wa Serikali ya Awamu ya Tano ambaye wakati wa kampeni zake aliwaahidi neema.

Kauli hiyo imekuja wakati takribani nyumba 16,000 zimeshawekewa alama ya kutakiwa kubomolewa na tayari nyumba 700 zikiwa zimebomolewa jijini Dar es Salaam, hali iliyowaacha baadhi ya wakazi wakiwa hawana sehemu za kujihifadhi, baadhi kupoteza fahamu na wengine kufungua kesi Mahakama Kuu.

“NEMC wasiwe kama wameshuka kutoka mbinguni na kukuta watu wamejenga mabondeni. Wasituharibie imani ya wananchi kwa Rais,” alisema Bulembo ambaye alikuwa na Magufuli katika kampeni za nchi nzima na kuwezesha CCM kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

“Kwani (NEMC) walikuwa wapi siku zote mpaka wafanye shughuli hiyo sasa baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani? Sikubaliani na bomoabomoa hiyo isipokuwa hiyo ya Jangwani na sehemu hatarishi za Bonde la Msimbazi.”

Kwa nini Jangwani
Akijenga hoja yake ya kukubaliana na ubomoaji wa nyumba za Jangwani katika Bonde la Msimbazi, Bulembo alisema eneo hilo kwa sasa ni hatarishi, hasa kutokana na tishio la mvua za El Nino.
“Kuna maeneo hatarishi kama Jangwani na Bonde la Msimbazi, huko bomoabomoa hiyo iendelee,” alisema.

“Mbali na eneo la Jangwani kuwa hatarishi kwa usalama wa watu, baadhi ya wakazi wake waliwahi kuondolewa na kupewa viwanja eneo la Mabwepande, lakini wakaviuza na kurejea upya.
“Lakini maeneo mengine kama ya Ali Maua, kwa nini uwabomolee watu wakati hatujasikia wamepata mafuriko na watu hao wako hapo kwa miaka yote?”
Bulembo alisema kuna maeneo mengine ambayo kuna mabonde, lakini hayajawahi kuleta madhara kwa wananchi hivyo hakuna haja ya kuwabomolea nyumba watu wa maeneo hayo wakati wameishi kwa miaka zaidi ya 20 au 30.

“Kuna watu wamekaa mahali kwa miaka 24 au 30 hawajawahi kupata mafuriko, hata kama wapo karibu na bonde, lakini si eneo hatarishi kwanini wabomolewe? alihoji kiongozi huyo wa zamani wa soka nchini.
“NEMC waache kuleta hasira za wananchi kwa Rais wao, walikuwa wapi mpaka wanasubiri sasa,” alisema Bulembo.

Rais hapendi umaskini
Wakati wakazi hao wanaobomolewa nyumba mabondeni wakidai kuwa operesheni hiyo inawaondoa kwenye umaskini na kuwafanya mafukara, Bulembo alisema anaamini hata Rais hafurahii kuona walalahoi wakiteseka kwa kuwa hata wakati wa kampeni alionyesha kulisikitikia kundi hilo.
“Moja ya mambo yaliyomsikitisha Rais wakati wa kampeni ni umaskini wa Watanzania. Alisema anaomba kura za wanyonge na ndiyo maana aliahidi kuondoa kero mbalimbali, ikiwamo kodi za wafanyabiashara wadogo,” alisema.

Nyumba 16,000 kubomolewa
Wakati Bulembo akisema hayo, NEMC walikuwa wakiendelea na ubomoaji na uwekaji alama ya “X”, ikiathiri wananchi wengi zaidi baada ya idadi ya nyumba zinazopaswa kubomolewa kufikia zaidi ya 16,000.

Kwa wastani wa kaya moja kuwa na watu wanne na nyumba moja kuwa na kaya kuanzia tano, ubomoaji wa nyumba 16,000 utasababisha watu 300,000 kukosa makazi, huku wanafunzi walio mwaka wa mwisho wa elimu ya msingi na sekondari wakiathirika zaidi.
Hali hiyo imezidi kuwatia wasiwasi wakazi hao huku wengine wakiporomosha vilio na kuzimia kutokana na mawazo ya kukosa mbadala wa makazi.

Ofisa mwandamizi wa NEMC, Arnold Kisiraga aliwaambia wanahabari jana kuwa kati ya nyumba 16,000 tayari 700 zilizokuwapo bonde la Mkwajuni, Hananasif na Suna zimeshabomolewa.
Kisiraga alisema huenda idadi ya nyumba zitakazobomolewa itaongezeka kutokana na utaratibu unaoendelea wa kubaini zilizojengwa mabondeni na kwamba leo watahamia Kigogo baada ya jana kumaliza Ulongoni, Gongo la Mboto na Pugu Mnadani.

Kwa jana pekee, alisema walibaini nyumba 885 zinazopaswa kubomolewa kutokana na kujengwa katika mazingira hatarishi, ikilinganishwa na juzi wakati walipobaini nyumba 647 zilizokuwa bonde la Mto Msimbazi--kuanzia Stakishari, Ukonga hadi Gongo la Mboto. “Hili zoezi la uwekaji alama ni moja na lile la ubomoaji linaloendelea Kinondoni. Ni vizuri zaidi wakaondoka wenyewe baada ya kuwekewa alama. Huu muda wangetumia vizuri kujipanga kuondoka kwa sababu yale ni maeneo hatarishi,” alisema Kisiraga wakati wa uwekaji alama hizo. Kuhusu uchambuzi wa nyumba 681 zinazotakiwa kuachwa katika bomoabomoa kutokana na zuio la Mahakama Kuu, alisema wanaendelea kuzibainisha na watakapomaliza wataanza kuzibomoa haraka zile zisizohusika na kesi.

‘Ni msiba mkubwa’
Wakati uwekaji alama hiyo ukiendelea, vilio vilitanda na baadhi wakihoji tarehe rasmi ya kubolewa makazi yao.
Yunis Amos, mkazi wa Ulongoni aliangusha kilio baada ya kuona nyumba yake ikiwekwa alama.
“Ni msiba mkubwa sana,” alisema Yunus huku akishika kichwa.
“Presha hapa inapanda na kushuka. Tutaishije na watoto hawa na wengine ni yatima? Huyu Magufuli anataka tuishije?”
Mkazi wa Bangulo, Saida Ally yeye aliwajia juu vibarua wa NEMC wanaoweka alama hizo, akiuliza eneo la kwenda baada ya nyumba yake kubainishwa kuwa itabomolewa. “Wanasema nianze kutoa bati sasa, nizipeleke wapi? Wanasema utaratibu utafuata baadaye, ni muda gani tuwe tumehama na tutahamaje? Sehemu ya kwenda sisi hatuna labda wakibomoa tutaenda kulala kwa huyo mwenyekiti wetu wa mtaa, hakuna namna,” alisema.

Azimia kwa kushindwa kuhimili
Ofisa mipango miji wa Ilala, Alfred Mbyopo alisema wananchi wengi wametaharuki baada ya nyumba zao kuwekewa alama za kutakiwa kubomolewa na juzi kuna mkazi mmoja alizimia.
“Kuna taharuki kubwa sana katika operesheni hiyo. Juzi kuna bibi mmoja pale Ulongoni A nasikia alizimia kwa kushindwa kuhimili uchungu wa nyumba yake kuwekewa alama ya kubomolewa. Lakini sisi tunawaokoa na hatari ya baadaye,” alisema Mbyopo.

‘Kidogo leo naweza kula’
Wakati baadhi wakilia, kwa Erasto Nyakiegi, kwa mkazi wa Mtaa wa Mwanapindi, Bangulo, mambo yalikuwa tofauti baada ya kutoka kwenye ‘kifungo’ cha sintofahamu kutokana na nyumba yake kukoswakoswa na alama hiyo.
“Tulikuwa tukiishi kwa wasiwasi sana na familia yangu tukijua ni nyumba zote za mabondeni. Karibu mwezi mzima nilikuwa sina hamu ya kula wala kulala, lakini leo naona nipo huru zaidi kwa kuwa nyumba yangu ipo nje ya zinazotakiwa kubomolewa. Kidogo leo naweza kula,” alisema Nyakiegi.
Hata hivyo, Mbyopo ambaye yumo kwenye uwekaji alama hizo, alisema kuna uchimbaji mkubwa wa mchanga ambao umesababisha Mto Msimbazi kuzidi kuliwa kingo zake na kuwaingiza baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye maeneo salama, kukumbwa na bomoabomoa.

Ndalichako alipa siku saba Baraza la Mitihani

Add Comment


Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amelipa siku saba Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kutoa maelezo kwa kubadili mfumo wa kupanga madaraja ya matokeo ya kidato cha nne na sita, kutoka jumla ya pointi kwenda wastani wa pointi (GPA).

Aidha, waziri huyo aliyewahi kuwa katibu mtendaji wa Necta, kwa miaka tisa, amelitaka baraza hilo kueleza sababu za watahiniwa binafsi kuanza kufanya mitihani ya upimaji endelevu.
Maagizo hayo yalitolewa na Profesa Ndalichako alipokutana na menejimenti ya baraza hilo jana Dar es Salaam baada ya Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde kueleza kuwa walifanya mabadiliko hayo kutekeleza maelekezo kutoka Wizara ya Elimu.

“Hakikisheni mnakuwa na misingi mizuri ya kimaamuzi na msikubali kufanya maamuzi yasiyo na tija kwa Taifa letu,” alisema Profesa Ndalichako huku akitolea mfano jinsi alivyokataa kwa barua watahiniwa binafsi kufanya mtihani wa upimaji endelevu, wakati akiwa katibu mtendaji wa baraza hilo.

“Tunawapa wiki moja mtupe maelezo. Tunataka kujua ninyi kama Baraza mliona sababu gani za msingi kubadili huu mfumo; faida zake nini, na mliwashirikisha watu gani. Kazi ya kuhakikisha utendaji wa taasisi zetu unakuwa mzuri ndiyo imeanza,” alisema Profesa.

Majibizano
Sakata hilo lilianza baada ya Dk Msonde kueleza sababu za mabadiliko hayo, huku akisisitiza mara kadhaa kuwa lengo lilikuwa kurahisisha udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu.
“Yalikuwa maagizo ya kuzitaka taasisi zote za serikali na serikali yenyewe kuwa na mifumo inayofanana yaani mifumo ya matokeo ya Necta ihusishwe na mifumo ya udahili ya TCU (Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania) na Nacte (Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi),” alisema Dk Msonde.
Aliongeza; “Mfumo wa wastani wa pointi haujabadili chochote kuhusiana na mfumo wa jumla ya pointi. Tumeutumia katika matokeo ya kidato cha pili, cha nne na cha sita na haujaleta matatizo. Wananchi na wanafunzi wa ngazi zote wanauelewa.”

Majibu hayo yalimzindua Profesa Ndalichako na kuhoji, “Hivi ni lini TCU walisema kuna ugumu wa kudahili kwa sababu ya uwapo wa mfumo wa jumla ya pointi? Tueleze kulikuwa na athari gani awali mpaka muanze kutumia GPA?”

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Simon Msanjila akitoa ufafanuzi kuhusu udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu alisema, “Mfumo wa udahili unaangalia taaluma si GPA. Mtu kama anakwenda kusoma taaluma fulani wanatazama masomo aliyosoma tu. Kama anakwenda kusoma sayansi watatazama masomo ya sayansi aliyosoma.”
Kutokana na kukosekana majibu sahihi, ndipo Profesa Ndalichako alitoa agizo hilo, huku akisisitiza kuwa ili Wizara ilielewe baraza hilo, lazima litoe sababu za msingi badala ya hizo walizoeleza jana.
Kuhusu mtihani wa upimaji endelevu, Profesa Ndalichako alisema haiwezekani watahiniwa binafsi kila somo wakafanya mitihani miwili, na kwamba ikiwa Necta haitatoa majibu ya kuridhisha, mitihani ya upimaji endelevu itafutwa.

Awali, akizungumza na wafanyakazi wa baraza hilo, Profesa Ndalichako alipongeza utaratibu wa kutoa vyeti mbadala kwa waliopoteza vyeti vyao halisi.

Pia, alilitaka baraza hilo kuwasilisha majibu ya mitihani ya watahiniwa wote ili wizara iyapitie.
Alisisitiza kuwa wakati mwingine wanafunzi hushindwa kujibu chochote au kwa ufasaha kutokana na matatizo ya walimu.

Samatta ailetea heshima Tanzania

Add Comment
Usiku wa kuamkia leo January 8, 2016 Mtanzania Mbwana Samatta ametutoa kimasomaso baada ya kushinda Tuzo ya mchezaji bora Africa kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Africa. Tuzo hyo imekuwa ya heshima sana kwa Samatta na Tanzania kwa ujumla...