Sh20 bilioni kujenga soko, kituo Kibaha


Kibaha. Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani inatarajia kutumia kiasi cha Sh20 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa na kituo cha mabasi.

Ofisa Ardhi wa Mji wa Kibaha, Edward Mbara alisema juzi kuwa fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB).
Alisema hayo mbele ya Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha, Gladys Dyamvunye akijibu malalamiko ya wakazi mjini humo ya kusuasua kwa utekelezaji wa miradi hiyo zaidi ya miaka mitatu huku kukiwa hakuna dalili yoyote juu ya utekelezaji wake.
Mkazi wa Kibaha mjini, Enock Aidani alisema kuchelewa kwa ujenzi huo kunawakosesha fursa za maendeleo kwani hivi sasa wanafanyabaishara katika mazingira magumu.
Mbara alisema halmashauri imeshapitia taratibu zote ikiwamo Tamisemi ambako wanasubiri kupata vibali kabla ya utekelezaji wake kuanza. (Sanjito Msafiri)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »